Abstract:
Uvumbuzi kimsingi huwa unahusisha utambuzi wa vitu, hali na hali aambazo
zilikuwapo awali lakini zikawa ama hazijulikani au hazikuwa zimetambuliwa kwa
kupewa majina. Utambuzi huu hutumia lugha. Huku nikusema kuwa uvumbuzi
niutambulishaji wakitu ambacho hakikujulikana kikajulikana. Ni uwasilishaji
wamawazo kupitia uwazaji makinifu. Kwa kuwasilisha mawazo na maoni,
wavumbuzi huwa wanatambulisha kitu kwa kutumia lugha. Uwazaji unaotumia
lugha huwapa wavumbuzi uwezo wa kufikia taswira za kindani zilizojisetiri
kwenye bongo zao. Wanasayansi makini hutumia lugha kuunda upya mawazo na
maoni yao upya ili kuenda nana muktadha wa changamoto zinawasukuma
kuvumbua. Suala hili huzua mtiririko wamawazo ambao hujengeka kwenye
mawazo yao yaawali yaliyokuwa kwenye akilizao. Kwa hivyo ni wazi kwamba ili
kufikia maarifa yoyote mapya katika uvumbuzi nisharti kutumia lugha. Kutokana
na nafasi kubwa ya lugha katika uvumbuzi, inakisiwa kuwa umadhubutiwa sera ya
lugha katika taifa lolote nirutuba ya uvumbzi wa wanasayansi. Katika uchunguzi
huu, tunajiuliza, wanasayansi huvumbua chochote kipya au huwa wanatumia lugha
kutambulisha jambo, kitu, maarifa au mawazo yaliyokuwapo tayari? Na je, kipi cha
msingi zaidi katika uvumbuzi, sayansi au lugha? Ikiwa uvumbuzi huandamana na
kuwezeshwan alugha, je mwanasayansi yoyote anapaswa kuitwa mwanaisimu? Na
je, sera ya lugha katika mataifa ya Afrika inaathiri uvumbuzi? Maswali haya ndiyo
tutashughulikia katikautafiti huu. Uchanganuzi nauhakikiwa nafasi ya lugha katika
uvumbuzi wakisayansi na kiteknolojia utafanywa katika utafiti unao kusudiwa.
Matokeo ya utafiti huu yatatumiwa kupendekeza kwawashika dau kuimarisha sera
ya lugha katika bara la Afrika kama njia ya kuendeleza uvumbuzi.